1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Milipuko mikubwa yaitikisa tena Khartoum

10 Mei 2023

Milipuko mikubwa imeutikisa tena leo mji mkuu wa Khartoum, wakati mapigano kati ya majenerali wawili wanaozozana nchini Sudan yakiendelea kupamba moto licha ya mazungumzo nchini Saudi Arabia.

https://p.dw.com/p/4R8eP
Bado kunashuhudiwa milipuko ya hapa na pale mjini Khartoum nchini Sudan, wakati vikosi hasimu vinapoendelea kupambana nchini humo.
Bado kunashuhudiwa milipuko ya hapa na pale mjini Khartoum nchini Sudan, wakati vikosi hasimu vinapoendelea kupambana nchini humo.Picha: AFP

Wakaazi wa Khartoum wamesema milipuko miwili mikubwa ilisikika katika eneo pana la Khartoum usiku wa kuamkia leo. Majenerali wanaozozana -- mkuu wa majeshi Abdel Fatah al-Burhan na kamanda wa vikosi vya wanamgambo Mohammed Hamdan Daglo -- waliwatuma wajumbe nchini Saudi Arabia Jumamosi kwa kile wapatanishi wa Marekani na Saudi Arabia walisema ni mazungumzo ya utangulizi kabla ya majadiliano  kamili. Lakini hakuna tangazo lolote lililotolewa la kupigwa hatua katika mazungumzo hayo yanayofanyika katika mji wa bandari wa Jeddah katika Bahari ya Shamu. Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini New York alisema jana kuwa Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada Martin Griffiths ameondoka Jeddah baada ya kupendekeza tamko la ahadi kutoka kwa pande zote mbili za kuhakikisha upitishaji salama wa misaada ya kiutu.