Miito ya usitishaji vita Gaza yaendea kutolewa
23 Februari 2024Matangazo
Hayo yameripotiwa wakati kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh ameondoka Misri baada ya kufanya mazungumzo na maafisa wa taifa hilo kuhusu uwezekano wa makubaliano ya usitishaji vita kwa ubadilishanaji wa mateka wa Israel walioko mikononi mwao na wafungwa wa Palestina walioko magereza ya Israel kuachiliwa huru.
Wanadiplomasia wa Ulaya wamezidisha miito yao ya kutaka mapigano yasitishwe kama tahadhari dhidi ya mzozo wa kibinadamu unaozidi kuwa mbaya Ukanda wa Gaza.
Vita vya Gaza vilianza baada ya Hamas kufanya shambulizi baya kusini mwa Israel na kuua watu 1,200 na kuwashika mateka wengine 250.
Israel, Marekani, Umoja wa Ulaya miongoni mwa mataifa mengine huliorodhesha Hamas kuwa kundi la kigaidi.