1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili 17 yapatikana baada ya ajali ya helkopta ya Urusi

1 Septemba 2024

Timu ya waokozi, baada ya kutokea ajali ya helkopta imesema imefanikiwa kupata miili 17 baada ya helkpta hiyo iliyokuwa na abiria 22 kuanguka katika rasi ya Kamchatka huko katika maeneo ya mbali ya mashariki mwa Urusi.

https://p.dw.com/p/4k9LI
Nepal katika ajali ya helikopta ya Kathmandu
Wafanyakazi wa kikosi cha usalama wanawatafuta watu katika eneo la ajali ya helikopta nje kidogo ya Kathmandu, Nepal, Agosti 7, 2024.Picha: Navesh Chitrakar/REUTERS

Mamlaka katika eneo hilo la rasi ilisema helkopta hiyo ilitoweka muda mfupi Jumamosi baada ya kuruka  ikiwa na watalii 19 na wahudumu 3. Kupitia ukurasa wa telegram, Gavana wa Kamchatka Vladimir Solodov amesema mabaka ya helkopta hiyo yalionekana Asubuhi ya leo katika katika eneo la milima lenye urefu wa mita 900.

Ajali zinazohusisha ndege na helkopta ni za mara kwa mara katikaeneo la mashariki ya mbali la Urusi, ambalo lina watu wachache na ambapo maeneo mengi yanafikika kwa helikopta pekee.

Mwezi Agosti 2021, helikopta ya Mi-8 iliyokuwa na watu 16 wakiwemo watalii 13 ilianguka kwenye ziwa huko Kamchatka kutokana na mazingira ya kutoonekana vizuri, na kuua wanane.