Tarehe 26 Aprili 2024, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliadhimisha miaka sitini tangu kuasisiwa kwake kwa kuunganishwa mataifa mawili yaliyokuwa huru, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kuunda taifa moja ambalo limedumu kwa miaka 60 sasa. Je, Muungano huu umemaanisha nini kwa watu wa pande hizo mbili? Mohammed Khelef anaongoza Meza ya Duara kujadili miongo hiyo sita.