Mnamo Machi 11 mwaka 2011, kulishuhudiwa ajali katika kinu cha nyuklia cha Fukushima iliyosababisha maafa makubwa, baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi ambalo lilifuatiwa na mafuriko ya tsunami katika pwani ya mashariki ya Japan. Vinu 3 kati ya 6 vya nyuklia huko Fukushima Daiichi- viliharibiwa vibaya na hivyo kuanza kumwaga sumu ambayo ilikuwa hatari kwa maisha ya watu na mazingira.