Wafanyabiashara wa soko la kimataifa la Kariakoo nchini Tanzania, wamegoma wakiishinikiza serikali kutatua kero zao. Baadhi ya kero hizo ni utitiri wa kodi, biashara ndogo za wazawa kufanywa na wageni. Pia wanalalamikia usumbufu wa maafisa wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).