Mfalme wa Moroko tayari kuutatuwa mkwamo wa Sahara Magharibi
12 Oktoba 2024Matangazo
Akitoa hotuba yake ya kila mwake bungeni hapo jana, Mfalme huyo alisema uamuzi wa Marekani, Uhispania na Ufaransa kutambuwa mamlaka ya Moroko kwa Sahara Magharibi umechangia kuonesha uwezekano wa kupatikana kwa suluhu mapema zaidi.
Moroko inaichukulia Sahara Magharibi kuwa jimbo lake la kusini, lakini kwa muda wote wakaazi wa eneo hilo wanajitambuwa kuwa taifa tafauti wanaloliita Sahrawi, likiongozwa na chama cha ukombozi cha Polisario.
Soma zaidi: Maelfu waandamana Moroco kushinikiza kusitishwa mahusiano na Israel
Uamuzi wa mataifa ya Magharibi kuitambua Moroko kuwa na mamlaka ya eneo hilo, unahusishwa na kukubali kwa Mfalme Mohammed wa Nne kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Israel mnamo mwaka 2020.