Mfalme wa Morocco atoa msamaha kwa waandishi 3 waliofungwa
30 Julai 2024Watatu hao walikamatwa na kushtakiwa kwa uhalifu wa kingono na kufanya ushushushu katika kesi iliyokosolewa vikali na makundi ya kutetea waandishi habari.
Taarifa za msamaha huo zimetolewa na Wizara ya Sheria ya Morocco siku ya Jumatatu wakati taifa hilo lilikuwa linafanya maadhimisho ya siku ambayo Mfalme Mohammed VI alitawazwa kukalia kiti cha enzi.
Waandishi waliopata msamaha huo ni Omar Radi, Taoufik Bouachrine na Soulaimane Raissouni. Watatu hao walihukumiwa vifungo tofauti mnamo mwaka 2018 na 2021 kwa makosayaliyojumuisha ubakaji, usafirishaji haramu wa binadamu na unyayasaji wa kingono.
Makundi ya kutetea waandishi yalisema kesi dhidi yao zililenga kuwafunga midomo na kuwazuia kuikosoa serikali. Wote watatu wanafahamika kwa uandishi makini unaokosoa vikali utawala wa nchi hiyo na sera za serikali.