AfyaUingereza
Mfalme Charles III wa Uingereza agunduliwa na saratani
6 Februari 2024Matangazo
Mamlaka ya Kasri la Buckingham imeeleza kuwa saratani hiyo iligundulika wakati wa matibabu ya kawaida ya tezi dume na kwamba kwa sasa Mfalme huyo ameanza kupatiwa matibabu na atahitaji kupumzika.
Viongozi mbalimbali duniani wakiwemo rais wa Marekani Joe Biden, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na wengine kadhaa, wametuma salamu za kumtakia ahueni Mfalme huyo aliyechukua madaraka baada ya kifo cha mama yake Malkia Elisabeth mnamo Septemba 8 mwaka 2022, aliyeiaga dunia akiwa na umri wa miaka 96.