Mfalme Charles III kulihutubia bunge la Ujerumani
30 Machi 2023Ziara hiyo ya siku tatu nchini Ujerumani ni yake ya kwanza ya kigeni tangu alipokalia kiti cha Ufalme, na inatafsiriwa kama "ishara yenye nguvu" ya kujenga mahusiano ya baada ya Brexit na bara la Ulaya.
Mfalme Charles wa III awali alikutana na Kansela Olaf Scholz kabla ya kuelekea bungeni.
Mfalme wa Uingereza Charles lll aanza ziara ya kiserikali nchini Ujerumani
Akizungumza jana katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Frank-Walter Steinmeier, Charles alifisia kile alichokiita "thamani ya kudumu ya uhusiano wa Uingereza na Ujerumani."
Alisema uungaji mkono wa pamoja wa nchi hizo mbili kwa Ukraine katika vita vyake dhidi ya uchokozi usio na uchochezi wa Urusi unadhihirisha nia yao ya kulinda na kukuza maadili yao ya pamoja ya kidemokrasia.