1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles atoa heshima kwa wahanga wa vita Hamburg

31 Machi 2023

Mfalme Charles III leo ametoa heshima zake kwa zaidi ya watu 30,000 wengi wao Wajerumani, waliofariki dunia katika mlipuko wa mabomu wa Hamburg karibu miaka 80 iliyopita

https://p.dw.com/p/4PZAs
Deutschland l Besuch von König Charles an der Gedenkstätte der St. Nikolai-Kirche in Hamburg
Picha: Matthias Schrader/AP/picture alliance

Mfalme Charles III leo ametoa heshima zake kwa zaidi ya watu 30,000 wengi wao Wajerumani, waliofariki dunia katika mlipuko wa mabomu wa Hamburg karibu miaka 80 iliyopita.

Soma pia: Mfalme Charles III aonya usalama wa Ulaya uko hatarini katika hotuba yake kwa bunge la Ujerumani

Heshima hizo amezitoa wakati alipouzuru mji huo wa kaskazini katika hatua yake ya mwisho ya ziara yake Ujerumani. Mfalme Charles ameweka shada la maua katika kanisa lililoharibiwa la Mtakatifu Nikolai ambalo kwa sasa ni makumbusho.

Soma pia: Mfalme Charles III alihutubia bunge la Ujerumani, asifu msaada kwa Ukraine

Mashambulizi yaliyosababisha uharibifu katika kanisa hilo yalifanywa mnamo Julai 1943 na ndege za kijeshi za Uingereza na Marekani, yalikuwa ni katika kujibu mashambulizi ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kinazi wa Ujerumani kwa Uingereza.

Mashambulizi hayo yalisababisha moto mkubwa ulioharibu sehemu kubwa ya mji wa Hamburg.