Mexico yawahamisha raia wake 34 kutoka Haiti
2 Aprili 2024Katika mkutano na wanahabari, waziri wa mambo ya nje wa Mexico Alicia Barcena, amesema kuwa watoto saba na maafisa wanne wa kidiplomasia waliokuwa wakazi wa Haiti ni miongoni mwa waliohamishwa.
Soma pia:Mtaalam wa UN: Haiti inahitaji walinda amani 5,000 kukabiliana na magenge ya wahalifu
Serikali ilionyesha picha za raia wa Mexico wakipanda helikopta ili kupelekwa kwenye meli hiyo, kutokana na kufungwa kwa uwanja wa ndege waPort-au-Prince.
Barcena ameongeza kuwa operesheni maalumu ilihitajika kuwaokoa watu hao ambao tayari wako safarini kuelekea Mexico.
Haiti imekumbwa na machafuko tangu mwezi Februari
Haiti imekumbwa na mapigano yanayozidi kuongezeka tangu mwishoni mwa mwezi Februari, wakati magenge yenye silaha yalipoanzisha mashambulizi yaliyoratibiwa na kumtaka waziri mkuu Ariel Henry kujiuzulu.