1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel asisitiza kuhusu uhuru wa habari

24 Agosti 2018

Vyama vya kihafidhina vya Kansela Angela Merkel vinakabiliwa na tuhuma za kupuuza ongezeko la makundi ya itikadi kali katika jimbo la mashariki mwa Ujerumani la Saxony

https://p.dw.com/p/33gLK
Merkel bei Diskussion an der  Iwane-Dschawachischwili-Universität in Tiflis
Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Wizara ya mambo ya ndani ya Saxony imethibitisha kuwa polisi huyo alihudhuria maandamano ya kundi linalopinga Uislamu la PEGIDA Jumamosi iliyopita na aliwaripoti kwa polisi wanahabari wa televisheni waliokuwa kwenye maandandano hayo ambapo walizuiliwa kwa dakika 45.

Video ilimuonyesha mwanamme aliyekuwa na kofia ya rangi za bendera ya Ujerumani akiwazomea wahabari wa ZDF akipunga mikono yake mbele ya kamera, na kuwaambia wasirekodi na kuwaripoti kwa polisi.

Waziri mkuu wa jimbo la Saxony Michael Kretschmer, ambaye ni mwanachama mwandamizi katika chama cha Merkel cha Christian Democratic Union – CDU, alionekana kutetea hatua ya polisi.

Katika wakati ambapo Ujerumani inapambana kuwajumuisha katika jamii zaidi ya wahamiaji milioni moja, tukio hilo lilizusha wasiwasi kuhusu wanaounga mkono makundi ya itikadi kali miongoni mwa polisi, hasa katika iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki ya Wakomunisti, na kuhusu uhuru wa habari.

Screenshot Bericht Frontal 21 Pressefreiheit in Sachsen
Polisi waliwazuia wapiga picha katika maandamano ya PEGIDAPicha: ZDF/Frontal 21

Akizungumza wakati akiwa ziarani katika mji mkuu wa Georgia, Tbilisi, Merkel alisema haki ya kuandamana lazima ihakikishwe kikamilifu.

Watakaoshiriki katika maandamano lazima watarajie kurekodiwa na kumulikwa na vyombo vya habari, hivyo wanahabari lazima wawe huru kufanya kazi yao. uchunguzi kuhusu hilo unaendelea, lakini nasisitiza kuwa naunga mkono uhuru wa habari, na yeyote anayeshiriki katika maandamano lazima ajue kuwa atakuwa sehemu ya uhuru wa habari.

Naibu kiongozi wa chama cha Social Democrats – SPD ambacho kinagawana madaraka na CDU katika serikali ya shiriksiho, awali alikituhumu chama cha Merkel kwa kujipa fahari kupita kiasi. Ralf Stegner anasema chama cha CDU katika jimbo la Saxony kwa miaka mingi kinakanusha au kutoyachukulia kwa umakini mavuguvugu ya itikadi kali na machafuko. Hatua hiyo imeyafanya makundi hayo kunawiri jimboni humo bila kupingwa na hilo halikubaliki.

Waziri wa sharia Katarina Barley, pia kutoka SPD alisema matukio hayo yanatia wasiwasi na yanapaswa kushughulikiwa na kuondolewa haraka kikamilifu

Uhuru wa habari ni moja ya nguzo za demokrasia yetu na taifa letu la katiba yetu na shambulizi lolote dhidi ya uhuru wa habari halikubaliki. tutachunguza kwa makini kilichotokea Saxony.

Deutschland Bundeskabinett Katarina Barley
Waziri wa sheria wa Ujerumani Katarina BarleyPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Uamuzi wa Merkel wa mwaka wa 2015 wa kuwakaribisha karibu wahamiaji milioni moja, wengi wao wanaokimbia vita katika Mashariki ya Kati, ulichochea uungaji mkono wa makundi ya siasa kali kama vile PEGIDA na AfD ambacho sasa ni chama kikuu cha upinzani bungeni.

Kretschmer, ambaye anaikosoa sera ya uhamiaji ya Merkel, anakabiliwa na mtihani mkubwa katika uchaguzi wa majimbo mwaka ujao kuishikilia Saxony katika chama cha CDU.

Wanazi mamboleo wana historia kubwa jimboni Saxony, hasa katika mji mkuu Dresden, ambapo wao hukusanyika kila mwaka Februari 13 katika kumbukumbu ya mabomu ya wanajeshi washirika katika mji huo wakati wa Vita ya Pili ya Dunia ambayo yaliwauwa watu 25,000 na kuharibu majengo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: