Melania Trump aunga mkono haki ya kutoa mimba
4 Oktoba 2024Suala hilo ni mojawapo wa mambo nyeti lenye kugawa pande tofauti katika uchaguzi ujao.
Kulingana na dondoo kutoka kwenye kitabu chake hicho cha kumbukumbu, Melania ameandika kwamba "ni muhimu kuhakikisha kwamba wanawake wana uhuru katika kuamua kuwa na watoto kutokana na hali zao, bila kuingiliwa au kupata shinikizo kutoka kwa serikali."
Soma zaidi: Trump na mkewe waambukizwa virusi vya corona
Msimamo huu wa Melania, unatofautiana na ule wa mumewe Trump ambaye mara kwa mara hujipiga kifua kwamba mahakimu aliowachagua kuiongoza Mahakama Kuu nchini humo, walisafisha njia ya kufikisha mwisho haki ya kitaifa ya uavyaji mimba.
Timu ya kampeni ya mpinzani wa Trump, makamu wa rais Kamala Harris, imeitumia tofauti hiyo ya wazi kati ya Trump na mkewe kuhusiana na suala hilo kwa ajili ya kuvutia upande wao. Harris anaunga mkono uavyaji mimba.