Baada ya kuaandamwa kwa wahamiaji wa Kiafrika Tunisia na kusababisha wengi kuondoka kwa maboti ya wasafirishaji watu kwa magendo kuelekea Italia, raia wa nchi za Kiafrika bado wamebakia hawana makaazi wala ajira nchini humo. Kulingana na shirika la Wanasheria Wasio na Mipaka (ASF) nchini Tunisia, Takriban watu 850 wameripotiwa kukamatwa kiholela, kwa msingi wa rangi. Msikilize Saleh Mwanamilongo.