1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbio za kumsaka waziri mkuu mpya wa Uingereza

11 Julai 2022

Ahadi za kutoa punguzo la kodi zinazotolewa na wagombea wanaowania kumrithi waziri mkuu wa Uingereza Boris Jonhson zinatao kitisho kingine cha mfumuko wa bei nchini Uingereza.

https://p.dw.com/p/4DyRA
UK Fragen für den Premierminister | Boris Johnson
Picha: AFP

Mfuko wa bei ambao unaweza kuilazimisha benki kuu ya taifa hilo kuongeza viwango vya riba kwa kiasi kibubwa, hatua ambayo inaondosha uwezekano wa wowote wa kukuza uchumi wa taifa hilo. 

Wengi kati ya wagombea 11, wanaojaribu kujipambanua kama watetezi wa maadili ya jadi ya Wahafidhina ya utozaji kodi ndogo, wameahidi kupunguza mzigo wa kodi ambayo inatarajiwa kufikia kiwango chake cha juu zaidi tangu miaka ya 1940.

Zikitaja kidogo tu mipango ya kupunguza matumizi kufikia punguzo la kodi, ahadi hizo zinaashiria kuondoka zaidi kwenye zama za kubana matumizi, ambazo zilikuwa alama ya sera za Kihafdhina kwa sehemu kubwa ya muongo kabla mlipuko wa janga la virusi vya corona kuchochea ongezeko la kihistoria la matumizi, na madeni kwa taifa hilo.+

Boris Johnson kajiepusha kuegemea upande wowote

Großbritannien | Boris Johnson kündigt Rücktritt an
Waziri Mkuu Boris Johnson akirejea ofisiniPicha: Frank Augstein/AP/picture alliance

Wakati jitihada hizo za kumtafuta mrithi wake katika chama chake zikienedea Johnson mwenyewe ameonesha kutomuunga mkono mgombea yeyote wa kumrithi nafasi yake ya uongozi wa chama chama na serikali. "Sitaki kusema zaidi kuhusu yote hayo, kuna kinyang'anyiro kinachoendelea na hilo lazima litokee na nisingependa kuharibu nafasi ya mtu yeyote kwa kuonesha uungaji mkono wangu. Lazima niendelee kidogo na katika siku chache na wiki zilizosalia, kazi ya kikatiba ya Waziri Mkuu katika hali hii ni kutekeleza wajibu, kuendelea kutekeleza wajibu, na ndicho ninavyofanya."

Amesema jukumu lake kama waziri mkuu kwa sasa ni kukiacha chama kifanye uamuzi, na kuendelea kutekeleza ile miradi ambayo ilifanya kichaguliwe ili kuifanikisha. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 58 alitangaza kuachia nafasi yake kama kiongozi wa chama cha Conservative na waziri mkuu Alhamisi iliyopita, lakini anasalia katika ofisi ya serikali hadi apatikane mbadala wake.

Soma zaidi: Kutoka Brexit hadi Partygate, hatimaye Johnson ajiuzulu

Anguko la Waziri Mkuu Johson limekuwa la kushangaza,baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Desemba 2019. Alishinda kwa wingi wa viti 80 kulikotokana na ahadi ya kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Wingi wake bungeni ulimpa nguvu ya kufanya hivyo lakini baadae uongozi wake ukazongwa na mikururo ya kashfa hatua ambayo ilimfikisha hata kulipishwa faini na polisi.

Chanzo: RTR/AFP