Mazungumzo ya amani ya Afghanistan yaanza Iran
7 Julai 2021Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, ujumbe wa Taliban unaongozwa na Sher Mohammed Abbas Stanikzai wakati ule wa serikali ya Afghanistan ukiongozwa na aliyekuwa makamo wa rais wa zamani wa taifa hilo, Younus Qanoon.
Katika hafla ya ufunguzi wa mazungumzo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Javad Zarif pamoja na kuupokea vyema uamuzi wa hasimu wao Marekani kujiondoa nchini Afghanistan, taifa ambalo linapakana na Iran kwa upande wa mashariki lakini amewaonya viongozi wa kisiasa kwa kusema " Wakati huuu watu wa Afghanistan na viongozi wa kisiasa lazima wachukue uamuzi mgumu kwa ajili ya hatma ya taifa lao.
Zarif: Marekani imesababisha athari kubwa Afghanistan.
Zarif ameongeza kwa kusema kuwepo kwa majeshi ya Marekani kwa miongo miwili nchini humo kumesababisha uharibifu mkubwa. Iran imekuwa ikiyahifadhi makundi kadhaa ya wakimbizi na wafanyakazi wahamiaji kutoka Afghanistan na imekuwa na wasiwasi mkubwa na kuzorota kwa hali ya amani kunakoongezeka katika kipindi hiki.
Katika hatua nyingine huko ndani nchini Afghanistan Kundi la Taliban limefanya mashambulizi ya kwanza dhidi ya mji mkuu wa mkoa wa Badghis uliopo huko magharibi uitwao Qala-i-Naw, tangu kuanzisha kampeni kubwa ya mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali.
Akielezea shambulizi hilo kwa umma Gavana wa mkoa wa Badghis Hessamuddin Shams, amesema Taliban wameingia mji mkuu baada ya kufanikiwa kudhibiti kwa wilaya zote, na kuongeza kuwa mapigano makali yanaendelea ndani ya mji.
Urusi kujitosa katika kuisaidia serikali ya Afghanistan dhidi ya Taliban.
Kufuatia hali hiyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amesema serikali yake ipo tayari kumtetea mshirika wake wa kikanda, endapo italazimika. Akizungumza katika ziara yake ya Laos, alisema taifa hilo lipo tayari kuitumia kambi yake ya kijeshi ya Tajikistan, ambayo moja kati ya kambi zake kubwa nje ya mipaka ya Urusi katika kutekeleza wajibu huo wa kiusalama kwa Afghanistan.
Kauli ya Lavrov ni kama ya kutilia mkazo, nyingine kama hiyo ya Jumatatu iliyotolewa na Rais Vladimir Putin kwamba serikali italisadia taifa hilo la iliyokuwa Jamhuri ya Kisovieti, kuliupesha na anguko baada ya Majeshi ya Marekani na washirika wao wa Jumuia ya Kujihami ya NATO kuondoka.
Chanzo: AFP/RTR