1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo kuhusu mpaka kati ya Tanzania na Malawi yakwama

27 Agosti 2012

Baada ya mazungumzo kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa kugonga mwamba, Tanzania imesema mazungumzo mengine yatafanyika tarehe 10 mwezi ujao kujaribu tena kutatua mzozo uliopo.

https://p.dw.com/p/15xF1
Wavuvi katika ziwa Malawi
Wavuvi katika ziwa MalawiPicha: Matthias Bölinger

Katika mazungumzo yaliofanyika nchini Malawi mjini Mzuzu, Malawi ilitaka mzozo huo utatuliwe katika mahakama ya kimataifa ya ICJ.

Kutaka kujua zaidi juu ya mkutano huo Amina Abubakar amezungumza na Asayah Mwambene ambaye ni mkurugenzi wa idara ya habari na mawasiliano katika wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania:

(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Khelef