Miundombinu ya kijeshi 3,920 nchini Ukraine imeharibiwa
14 Machi 2022Uharibifu huo wa miuondombinu ya kijeshi nchi Ukraine umefanyika huku Urusi ikisema kuwa hiyo ni operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine. Msemaji wa Wizara ya Ulinzi nchini Ukraine Igor Konashenkov leo Jumatatu ameeleza juu ya tukio hilo baya lililoilenga miundoimbinu ya Ukraine amsesema jumla ya miundombinu 3,920 ya kijeshi hapa nchini Ukraine imeharibiwa, ikiwa ni pamoja na ndege zisizokuwa na rubani 143, vifaru 1,267, majukwaa ya kurushia makombora na mizinga 124, silaha za ardhini na mizinga 457 na magari maalum ya kijeshi yapatayo 1,028. Msemaji huyo wa wizara ya ulinzi ya Ukraine amesema pia mtu mmoja ameuawa baada ya jengo la makaazi ya watu kushambuliwa mjini Kiev.
Wakati huo huo, China imeilaumu Marekani kwa kueneza taarifa za kupotosha juu ya jukumu la China katika vita vya Ukraine. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Zhao Lijian, amesema Marekani imekuwa ikieneza taarifa hizo potofu kwa nia ovu. China imetoa tamko hilo kabla ya mazungumzo kati ya wajumbe wa nchi mbili za Ukraine na Urusi yanayotarajiwa kufanyika kwa njia ya video ambapo wajumbe wa pande hizo mbili watashiriki katika duru ya nne ya mazungumzo. Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak, amesema mazungumnzo hayo yatajikita zaidi katika kuyafikia makubaliano ya kusitisha mapigano, kuondolewa kwa wanajeshi na dhamana ya usalama kwa Ukraine.
Soma:Urusi yazidisha mashambulizi nchini Ukraine
Wakati ambapo mazungumzo hayo yakisubiriwa kuanza vikosi vya kijeshi vya Urusi vinaendelea na mashambulio kwa lengo la kuudhibiti mji mkuu wa Ukraine, Kiev. Milio ya mizinga imesikika katika vitongoji vya Kyiv siku ya Jumatatu baada ya mashambulio ya anga katika kambi ya kijeshi iliyo karibu na mpaka wa Poland nchi ambayo ni mwanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO.
Wakazi wa miji iliyozingirwa na wanajeshi wa Urusi wanaweka matumaini yao makubwa katika mazungumzo ya kidiplomasia ambayo wanaamni yanaweza kufungua njia kwa raia zaidi kuondoka au hata kupata vifaa na mahitaji ya dharura kama chakula, maji na dawa vitu ambavyo vinaendelea kuwa haba.
Vyanzo: AP/RTRE/DPA