Mawaziri wa Ulaya kujadili uungaji mkono kwa Ukraine
12 Desemba 2024Matangazo
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imeeleza kuwa mkutano huo unakusudia kupeleka ujumbe wa wazi wa kuendelea kuiunga mkono Ukraine kwa kuzingatia mabadiliko yajayo ya rais nchini Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha, pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika Berlin.
Mbali na kujadiliana kuhusu msaada wa kijeshi, kifedha na kiutu kwa Ukraine, wanadiplomasia hao pia watazungumzia hali ya maendeleo nchini Syria, na athari zake katika ukanda huo.
Mbali na Kallas na Sybiha, Baerbock amewakaribisha pia mawaziri wenzake kutoka Ufaransa, Poland, Italia, Uhispania na Uingereza.