Mawaziri wa nishati wa G7 kujadili miundombinu ya Ukraine
20 Septemba 2024Matangazo
Tangu uvamizi kamili wa Moscow mnamo Februari 2022, mifumo ya nishati ya Ukraine imekuwa ikilengwa na mashambulizi ya Urusi na kusababisha matatizo ya ugavi wa umeme.
Soma zaidi: Scholz: Mapendekezo ya Putin kuhusu Ukraine hayana uhalisia
Hayo yakiarifiwa, Umoja wa Ulaya umesema unalenga kuikopesha Ukraine kiasi cha dola bilioni 39 kutoka kwa mapato ya mali za Urusi yaliyozuiwa katika umoja huo.
Norway, kwa upande wake, imesema itaongeza msaada wa kiraia kwa Ukraine dola milioni 475 na kutanua mpango wake wa msaada kwa miaka mitatu hadi 2030.