JangaPeru
Mawaziri wa mataifa manne Amerika ya Kusini kujadili usalama
16 Januari 2024Matangazo
Tangazo kuhusu mkutano huo wa mwishoni mwa juma hilo limetolewa na waziri mkuu wa Peru, Alberto Otarola, alipozungumza na waandishi habari jana jioni.
Amesema mkutano huo utafanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Lima, mnamo Jumapili inayokuja na utawaleta pamoja mawaziri wa Peru, Bolivia, Colombia na Ecuador
Otarola amesema ni muhimu kwa nchi hizo nne kukomesha biashara ya dawa za kulevya inayovuka mipaka, ambayo "ndiyo inafadhili shughuli za magenge ya uhalifu yanayosababisha vurugu, mauaji na wasiwasi ikiwemo vurumai iliyoshuhudiwa hivi karibuni nchini Ecuador."
Mkutano huo utajadili njia za kubadilishana taarifa za kijasusi pamoja na ushirikiano zaidi baina ya vyombo vya usalama vya mataifa hayo jirani.