1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na China wazungumza

14 Juni 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken ametoa wito wa kuendelezwa mawasiliano wakati alipozungumza na Waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang.

https://p.dw.com/p/4SY3Z
Bildkombo Antony Blinken und Qin Gang
Picha: Vesa Moilanen/Lehtikuva//Hector Retamal/AFP/Getty Images

Mazungumzo yao ya simu yamefanyika kabla ya mkutano wa ana kwa ana mjini Beijing. Blinken amesema kuwa Marekani itaendelea kutumia mazungumzo ya kidiplomasia ili kutatua wasiwasi wake pamoja na maeneo ya kuwepo na ushirikiano.

Naye Qin aliihimiza Marekani kuwacha kuingilia mambo yake ya ndani na kuuathiri usalama wake. Qin alimwambia Blinken aheshimu masuala ya msingi ya China kama vile suala la Taiwan ambayo China inasema ni sehemu ya himaya yake. 

Soma pia: Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken atasafiri kuelekea China.

Mahusiano kati ya madola hayo mawili makubwa kiuchumi yamezorota katika miaka ya karibuni kuhusiana na suala la kisiwa cha Taiwan, biashara na haki za binaadamu, miongoni mwa mambo mengine.

Blinken anatarajiwa kuzuru Beijing Jumapili kwa mazungumzo yanayolenga kutuliza mvutano, baada ya ziara iliyokuwa imepangwa awali kufutwa ghafla mwezi Februari.