SiasaIndia
Mawaziri wa mambo ya nje wa G20 wakutana India
1 Machi 2023Matangazo
Mwanadiplomasia wa ngazi za juu wa India Vinay Kwatra anasema wana imani kwamba changamoto za kiuchumi zilizotokana na vita hivyo zitaangaziwa kwa usawa pia.
Soma pia:Mkutano wa G20 wamalizika bila makubaliano muhimu kuhusu vita vya Urusi na Ukraine
Mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe 40 wakiwemo mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, mwenzake wa Marekani Antony Blinken na Qin Gang wa China. Mazungumzo yatafanyika hapo kesho baada ya chakula cha jioni leo.
Kundi la G20 linajumuisha nchi saba tajiri zinazojumuisha muungano wa G7 pamoja na Urusi, China, India, Brazil, Australia na Saudi Arabia miongoni mwa nchi zengine.