1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswidi

Mauzo ya silaha yaliongezeka duniani mwaka 2023

2 Desemba 2024

Ripoti ya shirika la SIPRI yaonesha mapato ya mauzo ya silaha yaliongezeka mwaka uliopita kote ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4neqG
Mapato ya silaha yanajumuisha mauzo ya bidhaa za kijeshi na huduma nyingine.
Mapato ya silaha yanajumuisha mauzo ya bidhaa za kijeshi na huduma nyingine.Picha: Russian Defense Ministry Press Service/AP Photo/picture alliance

Hayo ni kulingana na ripoti mpya iliyotolewa hivi leo na taasisi ya kimataifa ya masuala ya Amani SIPRI ambayo imesema kampuni 100 za silaha ambazo ni kubwa zaidi duniani zilishuhudia ongezeko la mauzo yao ya silaha na kufikia zaidi ya dola bilioni 600.

SIPRI imesema ongezeko hilo limechochewa na mizozo inayoendelea duniani ikiwa ni pamoja na ule wa Ukraine, Gaza na Asia Mashariki.

Ripoti hiyo imesema makampuni ya Marekani yalichangia karibu nusu ya mapato ya silaha kote duniani.

Mapato ya silaha yanajumuisha mauzo ya bidhaa za kijeshi na huduma nyingine.

Taasisi ya SIPRI imesema kampuni nyingi za silaha ziliongeza utengenezaji wa bidhaa hizo, hatua ambayo huenda ikaendelea.