1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauritius yazuia upatikanaji huduma za mitandao ya kijamii

1 Novemba 2024

Mauritius imezuia leo huduma za mitandao ya kijamii, siku chache tu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu. Hayo ni wakati mvutano ukiongezeka kuhusu kashfa ya kuvujisha mawasiliano ya simu.

https://p.dw.com/p/4mTtx
Mitandao ya kijamii katika simu ya kisasa
Mitandao ya kijamii katika simu ya kisasaPicha: Jonathan Raa/NurPhoto/picture alliance

Mauritius imezuia leo huduma za mitandao ya kijamii, siku chache tu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu. Hayo ni wakati mvutano ukiongezeka kuhusu kashfa ya kuvujisha mawasiliano ya simu. Hatua hiyo ya kushtusha imetangazwa na kampuni ya simu EMTEL, ambayo imesema iliamriwa Alhamisi usiku na Mamlaka ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuzuia huduma za majukwaa yote ya mitandao ya kijamii. Hatua hiyo inatarajiwa kudumu hadi Novemba 11 siku moja baada ya uchaguzi.

Soma: Meta, TikTok na X, wabanwa kuhusu usalama mtandaoni

Ofisi ya Waziri Mkuu imesema kanda za sauti zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii katika wiki mbili zilizopita huenda zilihatarisha usalama wa nchi hiyo ya kisiwa cha Bahari Hindi. Mawasiliano hayo yaliwahusisha wanasiasa, polisi, wanasheria, waandishi habari, wanachama wa mashirika ya kijamii yalivujishwa tangu katikati ya Oktoba. Waziri Mkuu Pravind Kumar Jugnauth anatafuta muhula mwingine kama mkuu wa chama cha Militant Socialist Movement. Alirithi uwaziri mkuu kufuatia kifo cha babake mwaka wa 2017 na akaupa ushindi muungano wake katika uchaguzi miaka miwili baadaye.