1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumizi ya DW na Psiphon kukwepa udhibiti wa intaneti

22 Machi 2021

Udhibiti wa serikali wa mtandao wa Intaneti ni suala linaloendelea kutishia uhuru wa kujieleza. Tangu 2012, DW imetumia programu ya Psiphon kuwezesha upatikanaji wa maudhui yaliozuwiwa kutoka DW na majukwaa mengine.

https://p.dw.com/p/3qxVx
	
Zensurumgehung - Software Psiphon RU
Picha: O. Linow/DW

Moja ya malengo makuu ya DW ni kutetea uhuru wa kujieleza na upatikanaji huru wa habari kote ulimwenguni. Hata hivyo, moja ya vitisho vinavyoongezeka dhidi ya kanuni hizi ni udhibiti wa mtandao. Nchi zinaendelea kuzuia mitandao ya habari kama vile DW ambayo hutoa habari za kuaminika pamoja na kuzima mitandao ya kijamii inayokuza majadiliano.

Ili kuwaruhusu watumiaji katika nchi hizi kuyapata maudhui ya DW pamoja na ya mitandao mingine iliyozuwiliwa, DW imekuwa ikifanya kazi naPsiphon, kampuni ya kibiashara ya Canada, kutengeneza programu za kukwepa udhibiti ili kulinda uhuru wa vyombo vya habari.  

Psiphon hutoa App na programu za kompyuta zinazotoa mifumo tofauti ya kuepuka ukaguzi na kutumia server mbalimbali, server za uwakala na teknolojia za VPN. DW sasa inatoa fursa tofauti kwa watumiaji wa mitandao kutumia teknolojia za Psiphon kuyapata maudhui ambayo yalikuwa yamedhibitiwa.
 

Upatikanaji wa maudhui ya DW yaliozuwiwa kupitia App ya DW

Tangu mwaka 2020, program ya Psiphon imejumuishwa kwenye app ya DW kwa ajili ya simu zinazotumia teknolojia ya  Android na iOS, na kuyafanya mauadhui ya DW kupatikana katika mataifa yalio na upatikanaji mdogo wa intaneti.

Zensurumgehung - Software Psiphon
Watumiaji watapata kitufe cha kuamsha Proxy kwa kubonyeza setting ya Proxy  Picha: DW/O. Linow

Kwa kubonyeza tu kitufe, watumiaji nchini Iran na China - ambako DW imezuwiwa - wanaweza kupata maudhui kwa kuchochea kiungo cha Proxy kwenye app hiyo. Kufanya hivyo, bonyeza kwenye menu kitufe juu kushoto kwenye app ya DW, bonyeza "Proxy" na kisha bonyeza "Activate Proxy" (Tazama picha).

Fahamu kuwa Proxy hutumia teknolojia tofauti zinazoweza kuathiri kasi ya upakiaji wa App na kwamba matumizi ya Proxy huenda yakakiuka sheria katika baadhi ya mataifa.  App ya DW inaweza kupakuliwa aidha kupitia Apple Store (iOs) ama google Play Store (Android).


Pakua App ya DW hapo

Utumiajia wa app ya Psiphon ya DW kuzipata tovuti na majukwaa mengine yaliozuwiwa

Limekuwa jambo la kawaida kwa serikali kuzuwia majukwaa ya mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na mitandao mingine kama njia ya kuzima uwezo w akujieleza.

DW imekuwa ikishirikiana na Psiphon kutoa programu za kurahisisha upatikanaji wa maudhui mengine na majukwaa ambayo yanazuwiwa na wadhibiti wa intaneti.

Iwapo unakabiliwa na matatizo kama hayo, fikiria kutumia app ya Psiphon. Kuiongezea app hiyo kwenye simu yako (iOS/Android), tuma barua pepe kwa anwani ya  [email protected] ili kutumiwa kiunganishi cha kupakua.  

Infografik Censorship bypass app Psiphon download instructions
Kwa kupakua kiunganishi, tuma ujumbe usiokuwa na kitu kupitia: [email protected]

Ukitumia Psiphon kupitia DW, utaelekezwa kwanza kwenye tovuti ya DW. Kutoka hapo, unaweza kuendelea kwenye tovuti yoyote nyingine.