1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya ubunge Zimbabwe yaanza kutangazwa

Sylvia Mwehozi
25 Agosti 2023

Matokeo ya kwanza ya majimbo ya ubunge yameanza kutolewa katika uchaguzi wa Zimbabwe baada ya hitilafu zilizojitokeza kusababisha upigaji kura kurefushwa kwa siku ya pili.

https://p.dw.com/p/4VYak
Uchaguzi  wa Zimbabwe
Mwanamke akipiga kura katika kituo cha kupigia kura huko Kwekwe, Zimbabwe,Picha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Matokeo ya kwanza ya majimbo ya ubunge yameanza kutolewa katika uchaguzi wa Zimbabwebaada ya hitilafu zilizojitokeza kusababisha upigaji kura kurefushwa kwa siku ya pili katika baadhi ya vitongoji na wanaharakati wa mashirika ya kiraia kukamatwa.

Zoezi la upigaji kura liliendelea jana katika kata 40 ambazo uchaguzi ulichelewa kuanza, hii ikiwa ni kulingana na amri ya rais licha ya sheria ya Zimbabwe kutoa siku moja ya kupiga kura.

Upinzani Zimbabwe wadai kuwepo "wizi wa kura" uchaguzi mkuu

Ingawa kata hizo ni chini ya asilimia moja ya nchi hiyo, lakini zinajumuisha kata 11 zilizomo mjini Harare na zenye idadi kubwa ya wapiga kura. Hadi kufikia jana, majimbo takribani 10 ya ubunge kati ya 210 yalikuwa yameanza kutoa matokeo.