Matatizo ya afya na njaa kwa wanawake yajadiliwa Burundi
10 Oktoba 2022Kongamano hilo la wanawake viongonzi limeandaliwa na ofisi ya mke wa rais Bi Angeline Ndayishimiye, inayohusika na maendeleo, aliyebaini kuwa kongamano hilo ni njia muafaka ya kubadilishana mawazo katika dhamira ya kuboresha afya ya wanawake, watoto na vijana. Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa mataifa amewataka washiriki katika mkutano huo kuhakikisha wamepata njia za kukabiliana na sababu zinazo pelekea kuwepo kwa matatizo ya afya na kutokuwepo na lishe bora kwa wanawake na watoto.
Mada zinazo jadiliwa katika kongamano hili zinaonesha kuwa tayari mumeelewa kuwa hakuna maendeleo endelevu yanayoweza kupatikana pasi na kuwekeza ktika afya ya binaadam hususan ya wanawake, watoto na vijana balehe.
Changamoto za kinamama na watoto
Mama Salma Kikwete alyeiwakilisha Tanzania katika mkutano huo alibaini kuwa mkutano huo unao muhimu mkubwa katika ustawi wa jamii na ukuwaji wa watoto na vijana. Mama Salma Kikweten Salma Kikwete alibaini kuwa kufanyika kwa mkutano huu kunadhihirisha kuwa Burundi imerudi kusimama baada ya kupitia changamoto.
Makamu wa rais Prosper Bazombanza aliyezinduwa rasmi kongamno hilo alibaini kuwepo na matumaini kuwa maagizo ya kongamano hilo yatapelekea kuwepo na mikakati ya kuboresha afya ya wanawake, watoto na vijana. Tunayo matumaini kuwa maagizo mtakayofikia katika mkutano huu
yatapekea kuwepo na mikakati itakayopelekea kuboreshwa kwa afya na lishe kwa wanawake na watoto katika nchi zetu#
Wanaohudhuria mkutano huo ni wujumbe kutokana nchi za DRC, Tanzania, Sudan Kusini Guinea ya Ikweta, na wale kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa yanao husika na wanawake na watoto.