Matajiri Uganda wachangia dola milioni 50 kwa Israel, Gaza
14 Desemba 2023Hii ni takriban wiki ya kumi tangu kuzuka kwa mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa kundi la Hamas.
Nchini Uganda matajiri wamekusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa vita hivyo kati ya Israel na Hamas.
Hatua hiyo ni ishara ya kudhihirisha huruma zao kwa waathirika wa vita hivyokatika mataifa hayo mawili na pia kuepusha kuonekana kupendelea upande mmoja.
Soma pia:Nani atafadhili ujenzi mpya wa Gaza, karibu nusu ya majengo yake yamebomolewa au kuteketezwa kabisa
Kundi hilo la matajiri wanaotoka kwenye imani za dini mbalimbali na washirika wao wa kimataifa wametoa msaada wa dola milioni hamsini. Wameelezea kuwa pesa hizo zimechangishwa na matajiri wa Uganda na wenzao wa kutoka nchi mbalimbali.
Stephen Keddi, mkurugenzi wa wakfu wa Keddi amesema kwamba wakiwa na washirika wao wanatoa kiasi cha dola milioni hamsini kwa ajili ya waathirika wa vita katika mataifa hayo, "Kila nchi itapokea dola milioni 25 kununua magari ya kubeba wagonjwa, mahema chakula na mahitaji mengineyo."
Wajumbe kupeleka msaada huo na kuona hali halisi
Makundi mawili ya wajumbe yametumwa kwenye nchi hizo kuwasilisha misaada hiyo ya kifedha na kuelezea kuwa hatua hiyo ni ishara ya kudhihirisha huruma zao kwa waathirika wa vita hivyo ambavyo sasa vimedumu takribani wiki kumi tangu vilipoanza Oktoba 7.
Sheikh Miladu Kaluma kutoka msikiti wa Nakasero ni mmoja kati ya wale watakaokuwa kwenye ujumbe utakaowasilisha misaada hiyo kwa Palestina amesema vita vinavyoendelea si vita vya kidini.
"Naomba mwenyezi Mungu awaoneshe ukweli waachane na hivyo vita" Alisema shekhe huyo kauli ambayo iliungwa mkono na mchungaji Stephen Okware ambae nae atakuwa miongoni mwa wajumbe watakaowasilisha misaada Israel kwa kusema hatua hiyo ina maana kubwa kwa waathirika wa vita hivyo.
Siku ya Jumatatu, Baraza Kuu la Umoja Mataifa lilipiga kura kutaka vita hivyo vikomeshwe.