Mataifa ya Magharibi yataka msaada wa kiutu kuingizwa Sudan
19 Oktoba 2024Nchi hizo zilitaka kuondolewa kwa vikwazo vya usafiri kwenye mpaka wa Adre kutoka Chad, ambako Umoja wa Mataifa unasema malori yake yanasubiri ruhusa ya kuingia Sudan.
Nchi hizo pia zilitoa wito wa kufunguliwa kwa njia zote za mpakani bila kuweko kwa vizuizi vyovyote, hatua ambayo awali ilikuwa imekubaliwa na pande hizo mbili zinazozozana.
Soma pia: Wakimbizi wa Sudan hatarini kutokana na mapigano: HRW
Katika tamko hilo, lililotiwa saini na Kamishna wa Ulaya wa Udhibiti wa Migogoro, nchi hizo zilisema zinalaani kwamba licha ya dharura iliyoko, pande hizo za SAF na RSF zinaendelea kuzuia kuingizwa nchini humo kwa msaada wa kibinadamu.
Pande zote mbili zimeshtumiwa kwa uhalifu wa kivita ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia na kuzuia msaada wa kibinadamu.