Mataifa ya kusini mwa Afrika yakabiliwa na janga la njaa
16 Oktoba 2024Matangazo
Miezi kadhaa iliyopita, nchi tano ambazo ni Lesotho, Malawi, Namibia, Zambia, na Zimbabwe, zilitangaza hali ya janga la kitaifa kutokana na ukame ambao umeharibu mazao na kuangamiza mifugo.
Katika taarifa iliyotolewa leo ikiwa ni Siku ya Chakula Duniani, WFP imesema kuwa Angola na Msumbiji pia zimeathirika pakubwa na kuonya kuwa mgogoro huo unatarajiwa kuongezeka kuanzia mwezi huu wa Oktoba hadi kipindi kijacho cha mavuno mnamo Machi au Aprili mwaka ujao.
Msemaji wa WFP katika eneo la kusini mwa Afrika Tomson Phiri, amesema ukame wa kihistoria, umeathiri zaidi ya watu milioni 27 kote katika eneo hilo la kusini mwa Afrika na kwamba takriban watoto milioni 21 wanakabiliwa na utapiamlo.