1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya kiisalam yaikosoa Marekani katika vita ya Gaza

9 Desemba 2023

Wizara ya mambo ya nje ya Qatar imesema kwamba nchi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu zimetoa wito kwa Marekani kuchukua "jukumu pana" katika kuishinikiza Israel kukubali kusitisha mapigano katika vita vya Gaza.

https://p.dw.com/p/4ZyBg
Gazastreifen, Khan Yunis | Nach einem israelischen Luftangriff
Raia wa Palestina wanafanya shughuli za utafutaji na uokoaji huku kukiwa na uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya anga ya Israel.Picha: Ahmad Hasaballah/Getty Images

Wito huo umetolewa katika mkutano jijini Washington kati ya Mawaziri wa mambo ya nje wa Qatar, Misri, Jordan, Saudia, Palestina na Uturuki wakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Soma piaNchi za Kiarabu zilishinikiza kukomesha mapigano, huku Umoja wa Ulaya ukiongeza makamanda wawili wa Hamas kwenye orodha yake ya magaidi.

Wakati wa mazungumzo hayo wajumbe hao wamedhihirisha masikitiko yao baada ya Marekani kutumia kura ya turufu kupinga muswada wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Mawaziri hao ni wajumbe wa kamati ya mawaziri iliyoundwa ya dharura katika Mkutano wa kilele wa Waarabu na Waislamu, ulioandaliwa na Saudi Arabia mwezi uliopita kujadili hali ya ukanda wa Gaza.