1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mataifa ya Ghuba yatuma salamu kwa rais mpya wa Iran

6 Julai 2024

Viongozi mbalimbali wameenedela kutuma pongezi zao kwa mwanamageuzi wa Iran Masoud Pezeshkian kwa kushinda urais nchini humo katika duru ya pili

https://p.dw.com/p/4hy1T
Masoud Pezeshkian na Saeid Jalili.
Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkiana akiwa na Saeed Jalili ambaye pia alikuwa anagombea nafasi hiyo.Picha: IRIB

Viongozi mbalimbali wameenedela kutuma pongezi zao kwa mwanamageuzi wa Iran Masoud Pezeshkian kwa kushinda urais nchini humo katika duru ya pili.

Soma zaidi. Masoud Pezeshkian ashinda uchaguzi wa rais Iran

Saudi Arabia ambayo ni mpinzani wa Iran kieneo imekuwa nchi ya mwanzo kabisa kutoa pongezi zake. Shirika la habari la serikali ya Saudia limeripoti kwamba mfalme Salman anatarajia kuendeleza ushirikiano baina ya serikali za nchi hizo bila katika masuala ya usalama na amani.

Viongozi wengine wa muungano wa Ghuba unaoongozwa na Saudia pia walituma salamu zao kwa Pezeshkian ikiwemo viongozi wa mataifa ya Oman, Falme za Kiarabu, Qatar, Kuwait na Bahrain.

Masoud Pezeshkian amechagauliwa na Wairan kuwa rais wa nchi hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Ebrahim Rais aliyekufa katika ajali ya helikopta mwezi Mei mwaka huu.