Mashirika ya UN yasema Gaza yahitaji msaada zaidi wa dharura
15 Januari 2024Wakati wakuu hao wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani - WFP, la kuwahudumia watoto UNICEF na la Afya Ulimwenguni - W.H.O hawakuitaja moja kwa moja Israel, wamesema uingizwaji msaada unaathiriwa kutokana na kufunguliwa kwa vivuko vichache vya mpakani, mchakato unaojikokota wa ukaguzi wa malori na bidhaa zinaoingizwa Gaza, na mapigano yanayoendelea kote katika ukanda huo.
Mashirika hayo yamesema njia mpya za kuingia Gaza zinapaswa kufunguliwa, malori zaidi yanapaswa kuruhusiwa kuingia kila siku, na wafanyakazi wa misaada na wale wanaotafuta msaada wanapaswa kuruhusiwa kusafiri kwa usalama.
Hayo yanajiri wakati maafisa wa afya katika Ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na wanamgambo wa Hamas wakisema kuwa idadi ya vifo kutokana na vita kati ya Israel na Hamas imepindukia 24,000.