1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Mashirika ya misaada yatoa wito wa ufadhili kwa Yemen

6 Mei 2024

Takriban mashirika 200 ya misaada yametoa wito wa ufadhili ili kuziba pengo la Dola bilioni 2.3 katika msaada kwa Yemen iliyokumbwa na vita.

https://p.dw.com/p/4fYMO
Mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths
Mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Martin GriffithsPicha: Fabrice Coffrini/AFP

Mashirika hayo pia yameonya kuhusu uwezekano wa athari mbaya zaidi katika taifa hilo maskini zaidi kwenye Rasi ya Arabuni.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na mashirika hayo, yakiwemo kadhaa ya Umoja wa Mataifa, imeonya kwamba watu milioni 18.2, ambao ni zaidi ya nusu ya wakaazi wa Yemen, wanahitaji msaada baada ya miaka 9 ya vita baina ya waasi wa Kihouthi na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudia.

Wito huo umetolewa siku moja kabla ya kufanyika mkutano wa ngazi ya juu wa maafisa wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, kujadili mpango wa ufadhili kwa Yemen inayokabiliwa na mojawapo ya mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu.