1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Urusi yauwa 12 Zaporizhzhya

7 Desemba 2024

Mashambulizi ya mabomu yanayoongozwa kwa mashine yameuwa watu 12 katika mji wa kusini mashariki mwa Ukraine, Zaporizhzhya.

https://p.dw.com/p/4nrfD
Ukraine, Zaporizhzhya
Wanajeshi wa Ukraine kwenye mstari wa mbele wa mapigano katika eneo la Zaporizhzhya.Picha: Gian Marco Benedetto/AA/picture alliance

Rais Volodymyr Zelensky ameyaita mashambulizi hayo kuwa ni tendo jipya la kigaidi la Urusi, huku akisema watu wengine wanne wamejeruhiwa.

Kwenye mashambulizi mengine dhidi ya mji wa kusini mashariki wa Kryvyi, watu wawili wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa, kwa mujibu wa ujumbe wa Zelensky kupitia mtandao wa X.

Soma zaidi: Lavrov: Urusi itatumia kila kitu chini ya uwezo wake kuzuia kushindwa vita nchini Ukraine

Rais huyo wa Ukraine amemtuhumu mwenzake wa Urusi kwa kutokutaka kabisa majadiliano na badala yake anaendeleza vitisho na mashambulizi.

Mstari wa mbele wa mapambano kati ya Ukraine na Urusi unatenganishwa kwa masafa ya kilomita 30 kusini mashariki mwa mji wa Zaporizhzhya.

Ndege za Urusi zina uwezo wa kudondosha mabomu hayo kutoka masafa ya kilomita 50.