Mashambulizi ya Israel yapiga maghala ya makombora Syria
16 Desemba 2024Matangazo
Shirika hilo limesema mashambulio hayo ndio mabaya zaidi kufanywa na Israel ndani ya Syria tangu mwaka 2012. Israel imekuwa ikiishambulia kile ilichosema ni maeneo ya kijeshi ndani ya Syria baada ya kuangushwa utawala wa Bashar al Assad.
Soma pia: Israel yadhamiria kuongeza idadi ya watu eneo la Milima ya Golan
Jeshi la nchi hiyo pia limekalia eneo la usalama la mpakani na Syria,hatua inayokosolewa huku Israel ikishutumiwa kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha vita ya mwaka 1974.
Wakati huo huo ubalozi wa Marekani mjini Damascus umewashauri raia wake waondoke Syria kutokana na hali ya usalama kuendelea kuwa tete na kutotabirika.