1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Qatar yalaani mashambulizi ya anga ya Israel huko Rafah

27 Mei 2024

Mashambulizi mapya ya Israel katika mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah huenda yakawa kizingiti katika usitishwaji wa mapigano na makubaliano ya kuachiwa kwa mateka.

https://p.dw.com/p/4gKC3
Mashambizi | Ukanda wa Gaza, Rafah
Wapalestina wakitazama uharibifu baada ya shambulizi la anga la Israel kwenye kambi ya wakimbizi.Picha: Jehad Alshrafi/dpa/picture alliance

Haya yamesemwa leo na mpatanishi katika vita hivyo, Qatar.

Qatar nchi ambayo imewapa makao viongozi wa kundi la Hamas tangu mwaka 2012, imelaani mashambulizi ya anga ya Israel huko Rafah ambapo kulingana na mamlaka za afya Gaza yamesababisha vifo vya dazeni kadhaa za raia wa Palestina.

Nchi kadhaa za Kiarabu ikiwemo Kuwait, zimelaani mashambulizi hayo.

Mwendesha mashtaka mkuu katika jeshi la Israel, Meja Jenerali Yifat Tomer Yerushalmi, amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na shambulizi hilo ambalo amelielezea kuwa la kuhuzunisha.