1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulio ya RSF yauwa watu wawili Darfur

3 Desemba 2024

Watu wasiopungua sita wameuwawa baada ya wanamgambo wa RSF nchini Sudan kushambulia kambi moja kubwa ya watu wasiokuwa na makaazi Kaskazini mwa Darfur.

https://p.dw.com/p/4nh5a
Darfur
Mashambulio ya RSF yauwa watu wawili katika kambi ya wakimbizi DarfurPicha: AFP

Wanaharakati wamesema kambi ya ZamZam iliyoko kusini mwa mji mkuu wa jimbo hilo la Darfur ilishambuliwa kwa roketi na mabomu yaliyofyetuliwa kiholela na kusababisha vifo na majeruhi.

Timu ya madaktari wa shirika la madaktari wasiojali mipaka - MSF ilisema walipokea watu wanane waliojeruhiwa baadhi yao vibaya wakiwemo wanawake na watoto wadogo.

Wanamgambo wa RSF wa Sudan watuhumiwa kuwaua watu 40

Katika wiki za hivi karibuni wanamgambo wa RSF wameimarisha udhibiti wao katika mji wa El Fasehr wakifanya mashambulizi kwenye maeneo kadhaa dhidi ya jeshi la Sudan na makundi ya wanamgambo washirika wao.