Marekani yazuwia msaada wa kifedha Georgia
31 Julai 2024Matangazo
Katika taarifa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, amesema hatua za serikali ya Georgia dhidi ya demokrasia na taarifa za uongo haziambatani na kanuni za uanachama katika Umoja wa Ulaya na jumuiya ya kujihami ya NATO.
Blinken amesema hatua hiyo inahusisha msaada wa zaidi ya dola milioni 95 ambao unanufaisha moja kwa moja serikali ya Georgia.
Hata hivyo, Blinken amesema Marekani itaendeleza mipango yake ya usaidizi na shughuli zinazonufaisha watu wa Georgia kwa kuimarisha demokrasia, utawala wa sheria, vyombo huru vya habari na maendeleo ya kiuchumi.