1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLiberia

Marekani yawawekea vikwazo wanaodidimiza demokrasia Liberia

28 Septemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza vikwazo vya viza za kusafiri kwa watu wanaodhoofisha demokrasia nchini Liberia.

https://p.dw.com/p/4WvQQ
George Manneh Weah rais wa Liberia
George Manneh Weah rais wa LiberiaPicha: Peter Dejong/AP/picture alliance

Hayo yanajiri mnamo wakati taifa hilo linakaribia kufanya uchaguzi mwezi Oktoba. Blinken amesema kwenye taarifa iliyochapishwa na wizara yake kwamba sera ya vizuizi vya viza inawalenga baadhi ya watu ambao si wa serikalini.

Hata hivyo haijaweka wazi ni watu wangapi watakaozuiwa kwenda Marekani chini ya vizuizi hivyo. Taarifa hiyo imefafanua kwamba walengwa wa vizuizi hivyo ni wale wanaofanya udanganyifu au wizi katika mchakato wa uchaguzi, kuchochea vurugu au kujihusisha katika shughuli nyingine yoyote kwa nia ya kuathiri matokeo ya uchaguzi.