Marekani yapanga mkutano na Japan na Korea Kusini
1 Aprili 2024Matangazo
Taarifa za kuwepo kwa mkutano huo zimeripotiwa hii leo na vyombo vya habari vya Japan.
Miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kujadiliwa na viongozi hao ni pamoja na kuimarisha uwezo wa kuzuia ushawishi wa China unaoongezeka, kitisho cha nyuklia cha Korea Kaskazini na mahusiano ya kijeshi kati ya mataifa hayo na Urusi.
Soma pia: NATO yajitenga na kauli ya Macron ya kuingiza jeshi Ukraine
Hata hivyo si Japan wala Korea Kusini ambayo imethibitisha juu ya mkutano huo na Marekani.
Agosti mwaka jana, Rais Joe Biden wa Marekani aliwaalika viongozi wa Japan na Korea Kusini kwa mazungumzo sawa na hayo ambapo watatu hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi na kufanya mikutano ya kila mwaka.