Marekani yaonya uwezekano wa mauaji ya kimbari Sudan
30 Aprili 2024Matangazo
Thomas-Greenfield aliwaambia waandishi habari kwamba historia inajirudia katika eneo la Darfur kwa njia mbaya zaidi, huku akiongeza kuwa mji wa al-Fashir uko katika hatari ya kutumbukia katika mauaji ya halaiki.
Soma zaidi: Baraza la usalama lahimizwa lisaidie msaada upelekwe Sudan
Mjumbe huyo wa Marekani amesema wanajuwa kuwa pande zote mbili katika mzozo huo wa Sudan zinapokea msaada wa silaha na mahitaji mengine kuimarisha juhudi zao za kuendelea kuiharibu Sudan na kwamba wamewasiliana na wahusika kuhusu suala hilo ikiwa ni pamoja na washirika wao kutoka Umoja huo wa Falme za Kiarabu.