Marekani yalaani mauaji ya wapinzani nchini Msumbuji
22 Oktoba 2024Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller ilisema kuwa inalaani mauaji ya wakili Elvino Dias na mgombea ubunge wa Podemos Paulo Guambe na kuongeza kuwa inaungana na wito uliotolewa na vyama vyote vya upinzani nchini Msumbiji kuhimiza uchunguzi wa kina wa uhalifu huo. Wawili hao waliuawa wakati gari lao lilipozingirwa na magari mengine katika mji mkuu Maputo kabla ya uchaguzi uliofanyika oktoba 9.Msumbijiimeshuhudia machafuko baada ya ya zoezi la upigaji kura, huku polisi wa kutuliza ghasia wakiwatawanya umati wa watu mjini Maputo hapo jana wakipinga madai ya udanganyifu katika uchaguzi. Rais Filipe Nyusi baada ya mihula yake miwili anaachia ngazi lakini mgombea wa chama chake cha FRELIMO, Daniel Chapo, anatarajiwa kushinda katika matokeo ya uchaguzi ambayo yatatangazwa wiki hii.