SiasaIran
Marekani yaitaka Iran kutowapa silaha waasi wa Houthi
14 Mei 2024Matangazo
Naibu balozi wa Marekani Robert Wood katika Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, iwapo inataka kufanikiwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen basi haina budi kuionya Iran.
Wood ameeleza kuwa, Iran haiwezi kuendelea kujificha nyuma ya kivuli cha Wahouthi.
Soma pia: Marekani yashambulia maeneo ya Wahotuhi wa Yemen
Mwanadiplomasia huyo amesema kuna ushahidi wa kutosha kwamba Iran inawapa wapiganaji wa Kihouthi silaha za kisasa, hatua ambayo ni ukiukaji wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Marekani imesema kuwa wapiganaji wa Kihouthi wamefanya zaidi ya mashambulizi 50 dhidi ya Meli, wameikamata meli moja na kuizamisha nyengine tangu mwezi Novemba.