Marekani yaisamehe Somalia deni la zaidi ya dola bilioni 1
6 Novemba 2024Wakati wa hafla ya kutia saini makubaliano hayo ya pande mbili, Riley alisema kuwa msamaha huo ni sehemu kubwa zaidi ya deni jumla la dola bilioni 4.5 inazodaiwa Somaliana nchi nyingi ambalo lilisamehewa chini ya makubaliano na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia mwezi Desemba.
Egeh aishukuru Marekani kwa msaada wake kwa Somalia
Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, Egeh aliishukuru Marekani kwa msaada wake usioyumba wa mageuzi ya kiuchumi na ukuaji nchini Somalia.
Marekani yajieleza kuwa mshirika thabiti kwa watu wa Somalia
Ubalozi wa Marekani umesema msamaha huo wa deni ni mbali na dola bilioni 1.2 za misaada ya kimaendeleo, kiuchumi, kiusalama na ya kibinadamu ambayo Marekani imetoa kwaSomalia mwaka huu, ikiielezea Marekani kama mshirika thabiti kwa watu wa Somalia.