1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaipunguzia Misri msaada wa kijeshi

Josephat Nyiro Charo10 Oktoba 2013

Baada ya miezi kadhaa ya kujivuta, Marekani imesitisha sehemu ya msaada wa kijeshi na wa kifedha kwa Misri kuashiria wasiwasi kuhusu umwagaji damu na ukosefu wa mchakato wa kuelekea utawala wa demokrasia nchini humo.

https://p.dw.com/p/19xFp
GettyImages 176918003 An Egyptian soldier is seen manning an armoured personnel carrier (APC) outside the Egyptian Constitutional Court in Cairo on August 19, 2013, while militants elsewhere killed 25 policemen in the deadliest attack of its kind in years, as Egypt's army-installed rulers escalated a campaign to crush supporters of ousted president Mohamed Morsi's Muslim Brotherhood. The assailants fired rocket-propelled grenades at two buses carrying police in the Sinai Peninsula, sources said, just hours after 37 Brotherhood prisoners died in police custody. AFP PHOTO/KHALED DESOUKI (Photo credit should read KHALED DESOUKI/AFP/Getty Images)
Marekani imeahidi kuendelea kutoa mafunzo kwa jeshi la MisriPicha: Khaled Desouki/AFP/Getty Images

Uamuzi huo uliwasilishwa jana katika mawasiliano ya simu ya dakika 40 kati ya waziri wa ulinzi wa Marekani, Chuck Hagel, na kiongozi wa kijeshi wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi. Hagel amesema Marekani imesitisha usafirishaji wa baadhi ya silaha za kijeshi na kusitisha msaada wa dola milioni 260 kwa viongozi wa kijeshi wa Misri, wanaoingoza nchi baada ya kumuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia, Mohammed Morsi, mwezi Julai mwaka huu.

Maafisa wa Marekani wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa uamuzi huo utazuia usafirishaji wa helikopta aina ya Apache, ndege za kivita aina ya F-16, sehemu ya vifaru aina ya M1A1 na makombora aina ya Harpoon. Hawakutoa takwimu maalumu, lakini wakasema thamani ya mikataba iliyositishwa itafikia mamia ya mamilioni ya dola ya msaada wa kijeshi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, Jen Psaki, amesema, "Ingawa hatua hiyo ya kudurusu upya sera iliyokuwepo kwa miongo kadhaa haitadumu, itaendelea kubakia kusubiri ufanisi wa maana utakaopatikana katika kuunda serikali itakayochaguliwa kupitia uchaguzi huru na wa haki na itakayowawakilisha Wamisri wote."

ARCHIV - Ein US-Kampfjet vom Typ F-16 Falcon startet zu einem Überführungsflug Richtung USA von der US Airbase Spangdahlem bei Trier (Archivfoto vom 27.04.2010). Die USA wollen F-16-Kampfflugzeuge sowie Transportmaschinen vom Typ Hercules nach Polen verlegen. Das sagte der polnische Verteidigungsminister Bogdan Klich nach Angaben der Nachrichtenagentur PAP am Samstag (04.12.2010) in Krakau. Laut polnischem Fernsehen TVP sollen die US-Maschinen 2013 nach Polen verlegt werden. Die Maschinen samt US-Besatzungen sowie Bodenpersonal sollen aber nicht dauerhaft bleiben, sondern in regelmäßigen Abständen ausgetauscht werden. Laut PAP will der polnische Präsident Bronislaw Komorowski bei seinem Besuch in der kommenden Woche in den USA auch über eine engere militärische Zusammenarbeit sprechenFoto: Boris Roessler +++(c) dpa - Bildfunk+++
Ndege ya kivita aina ya F-16Picha: picture-alliance/dpa

Psaki hata hivyo amesema Marekani itaendelea kuisaidia Misri kuilinda mipaka yake, kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi na uingizwaji wa silaha na kuhakikisha kuna usalama katika eneo la Sinai. Marekani pia itaendelea kuipa Misri vipuri kwa ajili ya vifaa vya kijeshi kutoka Marekani na kutoa elimu na mafunzo ya kijeshi, pamoja na misaada kwa ajili ya miradi ya afya, elimu na kuiendeleza sekta binafsi.

Seneta wa chama cha Democratic, Patrick Leahy, ambaye ni mwenyekiti wa jopo la baraza la seneti linalosimamia utoaji wa msaada wa Marekani kwa Misri, amesema uamuzi huo umepitwa na wakatiikizingatiwa matukio ya mwezi Julai. "Sheria yetu iko wazi.Wakati kunapofanyika mapinduzi ya kijeshi, msaada wa Marekani kwa serikali husika husitishwa," amesema Leahy katika taarifa yake.

"Badala ya kuhimiza maridhiano na kurejesha tena demokrasia kama ulivyoahidi, utawala wa kijeshi wa Misri umerudisha tena sheria za kijeshi na kuukandamiza upinzani wa wafuasi wa chama cha Udugu wa Kiismalu, ambao pia wametumia machafuko," akaongeza kusema Leahy.

Marekani kuendelea kushirikiana na Misri

Maafisa wamesisitiza kwamba serikali ya Marekani inauthamini sana uhusiano wake wa muda mrefu na Misri na haitasitisha misaada yote, ambayo kati yao dola bilioni 1.3 zimekuwa zikitengwa kwa ajili ya silaha za jeshi na mafunzo.

Akizungumza na waandishi wa habari afisa wa ngazi ya juu wa utawala wa Marekani amesema, "Uamuzi huu unasisitiza kwamba Marekani haitaunga mkono vitendo vinavyokwenda kinyume na maslahi yetu na kanuni zetu, na ni muhimu kuwa wazi kuhusu masuala hayo. Tumeuwasilisha ujumbe huo kwa uwazi kabisa na mara kwa mara kwa serikali ya Misri." Afisa mwingine wa serikali amesema Marekani sasa itashirikiana na Misri kuifanyia mageuzi mipango iliyopo ya msaada wa kiuchumi ijikite zaidi katika kuwanufaisha moja kwa moja Wamisri.

US Secretary of Defense Chuck Hagel speaks about the Defense budget at the National Defense University at Fort McNair in Washington, DC, April 3, 2013. Hagel warned Wednesday of deeper cuts to personnel, health care and weapons systems across his department, in order to put the brakes on spiraling costs and reshape the military for leaner budgets and new challenges. AFP PHOTO / Saul LOEB (Photo credit should read SAUL LOEB/AFP/Getty Images)
Waziri wa ulinzi wa Marekani, Chuck HagelPicha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Israel, ambayo inataka kuuendeleza mkataba wa amani wa mwaka 1979 na Misri, ilikuwa imeiomba Marekani iendelee kuisaidia serikali ya mpito ya Misri inayoongozwa na jeshi. Katika kuandaa orodha ya msaada wa kijeshi, utawala wa Obama ulizipa kipaumbele juhudi za kupambana na ugaidi, hususan katika eneo la Sinai na usalama wa mpakani.

Suala la mapinduzi ya kijeshi

Hatima ya msaada wa Marekani kwa Misri ilitiliwa shaka mweziJulai mwaka huu wakati jeshi lilipomtimua rais Morsi. Mapinduzi hayo yalifuatiwa na maandamano ya wafuasi wake, ambayo yalivunjwa kwa nguvu na jeshi. Utawala wa mjini Washington haukuileza hatua hiyo kama mapinduzi ya kijeshi. Morsi na wanachama wengine wa chama cha Udugu wa Kiislamu walikamatwa na bado wanazuiliwa. Mosri anashtakiwa kwa kuchochea machafuko dhidi ya waandamanaji alipokuwa madarakani na kesi yake itasikilizwa Novemba 4 mwaka huu.

Marekani imekuwa ikitaka Mosri aachiwe huru, na kesi yake huenda ikachochea machafuko zaidi ya wafuasi wake waliokabiliana na maafisa wa usalama Jumapili iliyopita ambapo watu 57 waliuwawa. Rais wa Marekani, Barack Obama, na wapambe wake mara kwa mara wameutaka utawala wa kijeshi wa Misri kuandaa uchaguzi mpya kurejesha utawala wa kidemorasia.

Mwandishi: Josephat Charo/AFPE

Mhariri: Daniel Gakuba