SiasaUrusi
Marekani yaionya Korea Kaskazini juu ya kuiuzia silaha Urusi
31 Agosti 2023Matangazo
Utawala wa Rais Joe Biden umesema kuwa, Urusi na Korea Kaskazini zinajadiliana juu ya makubaliano ya silaha.
Msemaji wa baraza la usalama wa kitaifa wa Marekani John Kirby amesema waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu hivi karibuni alisafiri hadi Korea Kaskazini ili kuishawishi nchi hiyo kuiuzia Urusi silaha.
Kirby ameongeza kuwa, tangu ziara hiyo, Rais wa Urusi Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamekuwa wakiandikiana barua, na kuahidi kuongeza ushirikiano kati yao.
Marekani imekuwa ikiwaonya wapinzani wake ikiwemo China juu ya kuisaidia Urusi katika vita vyake nchini Ukraine.