1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMyanmar

Marekani yaikosoa Myanmar kuongeza hali ya hatari

2 Februari 2023

Marekani imekosoa vikali hatua ya utawala wa kijeshi wa Myanmar kurefusha sheria ya hali ya hatari, ikisema inaongeza mateso ya miaka miwili baada ya mapinduzi ya kijeshi yalioiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa

https://p.dw.com/p/4N0RC
Philippinen Protest gegen Hinrichtungen in Myanmar
Picha: Edd Castro/Pacific Press/picture alliance

Marekani imekosoa vikali hatua ya utawala wa kijeshi wa Myanmar kurefusha sheria ya hali ya hatari, ikisema inaongeza mateso ya miaka miwili baada ya mapinduzi ya kijeshi yalioiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani, Ned Price amesema hatua hiyo inaendeleza utawala usio halali Myanmar na mateso inayoyaweka kwenye nchi hiyo.

Hapo jana, katika kukumbuku ya miaka miwili tangu yalipofanyika mapinduzi, utawala wa kijeshi ulisema unarefusha sheria hiyo kwa miezi sita zaidi, na hivyo kuchelewesha uchaguzi ambao utawala huo uliahidi utafanyika ifikapo mwezi Agosti.

Mapema jana, Marekani ilitangaza kuweka vikwazo zaidi kwa kampuni za biashara ya madini ya Myanmar, pamoja na maafisa wa kijeshi na wataalamu wa masuala ya nishati, kama sehemu ya juhudi za kuweka shinikizo zaidi kwa utawala wa kijeshi.